Watu laki tatu hawakurudi chanjo ya Uviko 19

DAR ES SALAAM: Wananchi 313,269 wa Dar es Salaam hawakurudi kupata chanjo ya pili ya Covid 19 tangu chanjo hizo zilipoanza kutolewa mwaka 2021.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Chanjo kutoka Manispaa ya Ubungo Hezron Msongole katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari jinsi ya kuripoti habari za afya ikiwamo chanjo ya ziada za Covid 19 yaliyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA).
Amesema, chanjo ya J&J waliochomwa jumla ni watu 2, 271,698 ambapo chanjo hii inachomwa dozi moja.
Amesema, waliochomwa chanjo ya Pfizer dozi ya kwanza ni 822,090 lakini waliorudi kwa ajili ya chanjo ya pili ni 678,492 hivyo watu 143,598 hawakurudi kupata chanjo ya pili ili kukamilisha.
Chanjo ya Sinopharm waliochoma dozi ya kwanza ni 506,514 waliorudi dozi ya pili ni 410,057 watu 96,457 hawakurudi kukamilisha dozi ya pili.
Kwa upande wa chanjo ya Moderna waliochoma dozi ya kwanza ni 70,501 waliorudi kukamilisha dozi ya pili ni watu 50,156 hivyo watu 20, 345 hawakukamilisha dozi wakati chanjo ya Sinovac dozi ya kwanza walichoma watu 327,876 waliokamilisha dozi ni watu 275,007 watu 52,869 hawakurudi kukamilisha dozi ya pili.
Msongole, amesema licha ya idadi kubwa ya watu kutorudia chanjo ya pili hata hivyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam umevuka lengo ambapo walitarajia kuwachoma chanjo watu 3,310,079 lakini walivuka na kuwachoma watu 3,685,410.
“Tulijitaidi kuwafuatilia na kuwataka kuja kurudia chanjo ili kukamilisha chanjo ya pili lakini wengi wao walitokomea hawakurudi,”amesema.
Amesisitiza kuwa Watanzania wengi huwa hawapendi kuchanja, na wengi waliochanja chanjo ya Covid hawarudi kupata Booster ambayo ni nyongeza ya chanjo ya kwanza.
3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *