7 wapoteza maisha California

Watu saba wameripotiwa kuuawa na mmoja kujeruhiwa katika matukio mawili ya ufyatulianaji risasi yanayohusiana na shamba la uyoga na kampuni ya magari aina ya lori katika jamii ya watu wa pwani kaskazini mwa California nchini Marekani, imeripotiwa watuhumiwa wamewekwa kizuizini.

Tukio hilo limetokea zikiwa zimepita siku mbili tangu kutokea tukio la mtu mmoja kuwaua watu 11 kwenye sherehe ya mwaka mpya wa Lunar karibu na Los Angeles, California, Jumamosi usiku.

Rais wa Bodi ya Wasimamizi wa Kaunti ya San Mateo, Dave Pine amesema watu wanne waliuawa katika shamba la uyoga na watatu katika biashara ya lori nje kidogo ya Half Moon Bay, mji ulio umbali wa kilomita 48 (maili 30) kusini mwa San Francisco.

Pine alisema mtuhumiwa alifanya biashara na kutoridhishwa na makubaliano baina ya pande mbili za biashara hiyo. Ofisi ya Sherifu wa Kaunti ya San Mateo iliandika kwenye kwamba mshukiwa alikuwa kizuizini.

Habari Zifananazo

Back to top button