Watu tisa kupatiwa huduma mpya MOI

TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) iliyopo jijini Dar es Salaam itaanza kutoa huduma mpya ya utoaji wa nyama za uvimbe katika ubongo kwa ajili ya vipimo na matibabu kwa njia ya tundu dogo kupitia vifaa maalum ambapo watu tisa wanatarajiwa kupatiwa huduma.

Awali aina hiyo ya huduma ilikuwa inafanyika kwa njia ya pua ambapo mgonjwa huongiziwa mirija kupitia pua na kutolewa nyama za uvimbe.

Akizungumza wakati wa mafunzo y ambayo yalianza kutolewa leo ambapo huduma hiyo itatolewa Februari 22,2024 kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Colorado iliyopo nchini Marekani, Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo na Mgongo wa MOI, Dk Lemeri Mchome alisema huduma hiyo ni mara ya kwanza kutolewa kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Upasuaji unatarajiwa kufanywa kwa wagonjwa watatu ambao wanauvimbe kwenye uti wa mgongo,watatu ambao walitakiwa kufanyiwa upasuaji kwa njia ya pua na watatu ambao walitakiwa kufunguliwa fuvu na kutolewa uvimbe kichwani.

“Huu ni mkutano wa tatu ambao ni ushirikiano kati ya MOI na hospital ya Chuo cha Colorado Marekani ushirikiano ulioanza 2017 katika upasuaji wa vivimbe hasa tulianza na ule wa njia ya pua ni faida kubwa tuliyopta kutoka kwao.

Ameongeza “Tunaanza tiba mpya ambayo ni yakuchukua vinyama ndani ya ubongo bila kufungua tundu kubwa tunatumia tundu dogo sana tutapitisha vifaa na kupata vinyama vya kwenda kufanya vipimo na matibabu.

Dk Mchome amesema huduma hiyo piq itawasaidia kwenye matibabu ya magonjwa mengi kama kutetemeka ,kutembea na kushindwa kudhibiti mwili kwani zinapatikana kupitia kifaa walicholetewa.

Amesema MOI ina madaktri 13 ambao ni wabobezi katika upasuaji wa ubongo,uti wa mgongo na mishipa yafahamu na kuna wataalam maalum watatu wa kufanya upasuaji bila kufungua fuvu.

“Tulisoma elimu darasani lakini hatuna vitendo tumepanga baada ya hapa kuna wataalamu wataenda huko kujifunza zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button