Watu zaidi ya laki moja wagundulika na VVU 2023

22,000 wapoteza maisha

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema watu 163, 131 wamegundulika kuwa na maambukizi mapaya ya virusi vya ukimwi  (VVU) kwa mwaka 2023.

Ummy ameyasema hayo leo Januari 10, 2023 jijini Dar es Salaam akitoa  taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023.

Amesema, jumla ya watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) na Watu 163,131 kati yao walingundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Mkakati waandaliwa kupunguza maambukizi ya VVU

“Kwa upande wa ugonjwa wa UKIMWI, Serikali iliendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo katika mwaka 2023 jumla ya Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) kulinganisha na Watu 6,930,758 mwaka 2022 (DHIS2 2023),”amesema na kuongeza

“Kati ya watu waliopima mwaka 2023, watu 163,131 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU ukilinganisha na watu 182,095 mwaka 2022 (DHIS2 2023),”amesema

Aidha, amesema waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651 kulinganisha na watu 1,612,512 (DHIS2023)

“Mwaka 2023, vifo vitokanavyo na UKIMWI vilikuwa 22,000 kulinganisha na vifo 29,000 mwaka 2022(Spectrum 2022),”amesema Ummy.

Habari Zifananazo

Back to top button