MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru watu wawili waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la kumuua kwa kukusudia Issa Juma, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yao.
–
Washitakiwa hao Maulid Idd na Abuu Vunja wakazi wa Tandika Kilimahewa, wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Ramadhani Rugemalila, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya hukumu.
–
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rugemalila, alisema wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo upande wa mashitaka walipeleka mashahidi wanne na vielelezo vitatu, ambavyo vimeshindwa kuthibitisha shitaka dhidi yao.
–