Watuhumiwa 377 dawa za kulevya wahukumiwa

Nyumba, Magari, pikipiki, boti, zataifishwa

WATUHUMIWA  377 wametiwa  hatiani kwa makosa ya kujihusisha na madawa ya kulevya katika mahakama mbali mbali nchini Tanzania Bara na Visiwani.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 23, 2022 na Mkuu wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Amon Kakwale imesema kuwa  kuanzia mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakamani na kutolewa uamuzi.

Amesema katika maamuzi hayo, watuhumiwa 170 walifungwa vifungo mbalimbali kwa makosa hayo.

ACP Kakwale amesema pia Jeshi hilo lilikamata  vyombo vya moto na  nyumba na kuvitaifisha kuwa mali ya serikali.

Ametaja vilivyotaifishwa ni magari nane, Pikipiki tisa, Boti mbili na nyumba moja

“Jeshi hilo halita muonea muhali mtu yeyote atakae kamatwa akijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na linawaomba wananchi kutoa taarifa za watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ili hatua zichukuliwe dhidi yao.”Amesema

Habari Zifananazo

Back to top button