Watuhumiwa wanne wa ujambazi wadakwa Dar

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata majambazi sugu wanne maeneo ya Mabibo External na kwa sasa watuhumiwa hao wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza leo Januari 9,2023, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao hali zao ni mbaya baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati wakishambuliana na Polisi .
“Majambazi hao wamekamatwa Januari 8 mwaka huu wamekiwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora fedha katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaamna na mikoa ya jirani.” Amesema Muliro
Muliro amewataja viongozi wa watuhumiwa hao wa ujambazi sugu ni Athuman Mbalilo maarufu kwa jina Soti(50)Mkazi wa Kimara Temboni na Mpoki Raphael kwa jina lingine Mwangwisya(41) mkazi wa Mbezi Luis.