Watuhumiwa zaidi ya 300 mbaroni kwa uhalifu

MBEYA:  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 324 kwa tuhuma za kujihusisha na magenge ya uhalifu ikiwemo mauaji, wizi, utapeli, pombe haramu, uhalifu wa kimtandao na makosa ya usalama barabarani.

Watuhumiwa hao walikamatwa katika kipindi cha mwezi Aprili 2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Abdi Issango amewaeleza Waandishi wa Habari, Leo Mei 03, 2024.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi Jitegemee Christopher Peter [39] na Mwalimu George Ngalya [42] wa shule ya Msingi Mnyakongo zote za Mkoani Dodoma kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa TAMISEMI ambapo wanadaiwa kulaghai na kuwatapeli watu kwa madai kuwa wanatoa ajira Serikalini pamoja na mikopo kwenye serikali za mitaa.

Isome pia https://habarileo.co.tz/polisi-yanasa-mtandao-wezi-wa-magari-tanzania-malawi/

Watuhumiwa hao waliokamatwa katika Mji mdogo wa Mbalizi wakiwa katika nyumba ya kulala wageni na kukutwa na vitu mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya Taifa (NIDA), simu za mkononi tano, kishikwambi kimoja, simu aina ya Samsung moja pamoja na laini za simu 16 za mitandao mbalimbali zenye usajili wa majina tofauti tofauti.

Habari Zifananazo

Back to top button