Watuma maombi TRC uendeshaji wa reli

DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Reli nchini (TRC), limepokea maombi kutoka kampuni za uendeshaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika uendeshaji wa reli.

Hayo yameelezwa  na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa katika mtukano na  wahariri pamoja na  waandishi kwenye kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TRC na mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia.

Amesema serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017, ikiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utoaji huduma za usafirishaji kupitia miundombinu ya reli, hatua inayolenga kuchochea ushindani, ufanisi na ubunifu katika sekta hiyo.

Amesema jitihada za serikali katika kuwekeza sekta ya reli zimejikita kuboresha miundombinu ya reli iliyopo, ujenzi wa reli mpya ya kiwango cha Standard Gauge, na ununuzi wa vitendea kazi kama injini na mabehewa.

Habari Zifananazo

Back to top button