Watumiaji Intaneti wafikia milioni 34

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo katika taarifa yake ameeleza Watanzania 34.4 hadi sasa wanatumia huduma ya Intaneti.

Mkumbo ametoa takwimu hizo leo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Takwimu hizo zimeonesha ongezeko la watumiaji wa hudumu hiyo kwani mwaka 2010 watumiaji walikuwa milioni 15.2 kwa mujibu wa Prof Mkumbo.

Advertisement

Aidha watumiaji wa wanatumia mitandao ya kijamii nchini wamefikia milioni 16.7 ambapo watumiaji wa TikTok wamefikia milioni 1.6.

2 comments

Comments are closed.