Watumiaji internet China wafikia bilioni 1

IDADI ya watumiaji wa internet nchini China imefika bilioni 1.032  mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 83 ikilinganishwa na mwaka 2012, mapinduzi yaliyotokana na maboresho katika sekta ya mawasiliano nchini humo.

Maboresho hayo pia yamechangia katika ongezeko la mapato kufikia Sh trilioni 504.4 (Yuan trilioni 1.47) mwaka 2021 kutoka yoan trilioni 1.8 mwaka 2012.

Taarifa iliyochapishwa Ijumaa Agosti 19, 2022, imesema idadi ya programu za simu imefikia milioni 2.32.

Ofisa wa Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari, Xie Cun ameongeza kuwa China imejenga Mkongo mkubwa zaidi duniani na mtandao mkubwa kwa watumiaji wa rununu.

“Kuanzia mwaka 2012 hadi 2021, miundombinu ya mawasiliano ya China imepata maendeleo makubwa, na “mgawanyiko wa kidijitali” kati ya maeneo ya mijini na vijijini umepungua kwa kiasi kikubwa, “ Ofisa huyo alisema na kuongeza:.

“Katika hatua inayofuata, nchi itaimarisha zaidi msingi wa maendeleo ya tasnia ya habari na mawasiliano, kukuza vichocheo vipya vya ukuaji na kuwezesha mabadiliko ya kidijitali ya tasnia ya jadi, “ Xie alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button