Watumishi afya watakiwa kuzingatia maadili

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu, amewataka watumishi wa afya nchini  kuzingatia maadili, weledi na viapo vyao wanapotoa huduma kwa wananchi, ili kuondoa malalamiko.

Rai hiyo ameitoa leo wakati aliposhiriki shughuli ya usafi na upandaji miti katika Kituo cha Afya cha Makorora kilichopo jijini Tanga.

Advertisement

Amesema wakati huu serikali inavyoendelea kuboresha huduma za afya, lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila vikwanzo, hivyo ni wajibu wao wahudumu kutoa huduma bora.

“Serikali inazifanyia kazi changamoto zote katika sekta ya afya, ikiwemo upungufu wa watumishi wa afya, hivyo niwaombe licha ya uchache wenu timizeni wajibu wenu wa kutoa huduma kwa mujibu wa viapo vyenu,”amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora, Dk Angelina Mashaka amesema kuwa katika kipindi hiki cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita, upatikanaji wa dawa umekuwa wa uhakika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *