Watumishi Mbongwe wakaliwa kooni

wasisitizwa weledi, bidi

GEITA: WATUMISHI wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, wametakiwa kuwahudumia watanzania bila kuwabagua kwa namna yoyote ile.

Hayo yamesemwa leo Novemba 24, 2023 na Katibu Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS) ,Mohamed Gombati katika kikao kazi na watumishi wa halmashauri na watendaji wa taasisi za serikali wilayani humo.

Gombati amewakumbusha watumishi hao kuwajibika kwa umma kwa kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi zinatolewa ngazi zote za utawala ndani ya wilaya.

Aidha, amewataka watumsihi wa serikali kuongeza juhudi za kusimamia na kuhakikisha mapato ya Halmashauri ya Mbogwe yanaongezeka na kufikia malengo yaliyopangwa.

Awali, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe (DAS) Jacob Julius ‘Jaju’, akimkaribisha Gombati, amewaasa watendaji wenzake kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu kazi na dhamana walizopewa kwani wako watanzania wengi sana wanaotafuta kazi na dhamana hizo.

“Ni vyema kwa waliobahatika kupata fursa za kuwatumikia watanzania kwa nafasi na maeneo mbalimbali kuheshimu kazi na kuwatumikia wananchi kama ambavyo serikali inaelekeza,”amesema Julius.

Habari Zifananazo

Back to top button