“Watumishi msiogope mfumo wa HRA”

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Ridhiwani Kikwete amesema Mfumo wa Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HRA) hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.

Kikwete amebainisha hayo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.

Amesema lengo la mfumo huo ni kuwezesha kupima utendaji wa watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini.

“Mfumo huu hauna lengo la kukomoa watu, tunatakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupanga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia” amesema Kikwete.

Ameongeza mifumo hiyo inakwenda kuonesha wapi kwenye mapungufu ili paweze kuboreshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Prof. Abel Makubi akimkaribisha Naibu Waziri huyo alimpongeza kwa kuitembelea MOI mara kwa mara na kwamba hatua hiyo inaongeza ari kwa watumishi kufanya kazi kwa umahiri.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button