‘Watumishi rudisheni kwa jamii yenye uhitaji’

KATIKA maadhimisho ya kilele cha wiki ya utumishi wa  umma, taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali zimeshauriwa kuikumbuka jamii ya wenye uhitaji, ili kutimiza dhana ya utumishi bora.

Hayo yamesemwa na watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazini leo Juni 23, 2023 walipotembelea kambi ya wazee ya Nunge iliyopo Mtaa wa Majengo  Kigamboni, Dar es Salaam na kutoa mahitaji mbalimbali.

Mkurugenzi wa Ubinafsishaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mohamed Nyamasa amesema ni vyema jamii ikawakumbuka wenye uhitaji ambayo ni moja ya sifa za utumishi bora.

Advertisement

“Katika wiki hii ya utumishi wa umma tumefanya matukio mbalimbali ya kijamii, hili la leo la kufika hapa Nunge ni mwendelezo wa taasisi yetu kuendelea kukumbuka wenye uhitaji na hiyo ndio maana ya kuwa mtumishi bora,” amesema Nyamasa.

Wanufaika wa misaada iliyotolewa ambao ni wazee wanaoshi katika kambi hiyo, wamesema bado kuna changamoto nyingi hivyo wanaiomba jamii iwakumbuke.

” Tunashukuru kwa misaada hii , tunaamini itakwenda kutusaidia kwa kiasi kikubwa na tunaombwa tuendelee kukumbukwa,” wamesema kwa nyakati tofauti.

Ofisa Ustawi wa Jamii anaesimamia kituo hicho Jackina Kanyamwenge, anasema jamii ya wenye uhitaji inakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo haipaswi kusahaulika.

Kituo cha Nunge kipo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, kina jumla ya wenye uhitaji 21 wanawake 10 na wanaume 11

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *