Watumishi wa afya 10,462 waajiriwa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dk Festo Dugange amesema Serikali imeajiri watumishi wa kada za afya 10,462 Katika kipindi cha mwaka 2020/21 na 2021/22 na kuwapanga kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Uhitaji.

Dk Dugange amesema hayo leo tarehe 07 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini, Moshi Selemani Kakoso akiyetaka kujua Je, ni lini Serikali itapeleka wahudumu wa afya na madaktari kwenye vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya katika Wilaya ya Tanganyika.

Amesema kati ya ajira 7,612 za kada ya afya zilizotolewa na Serikali mwezi Julai, 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ilipangiwa watumishi 62 wa kada mbalimbali ikiwemo wauguzi na madaktari kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati.

Dk Dugange amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya na itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya na kuwapeleka katika vituo vya huduma kote nchini.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Gedion Kiswaga alitaka kujua Je, ni lini Serikali itajenga Maabara kwenye Zahanati zote za Jimbo la Kalenga

Wakati akijibu Swali hilo, Dk Dugange amesema Katika mwaka wa fedha 2021/22, serikali ilipeleka fedha shilingi bilioni 27.8 kukamilisha maboma ya zahanati 555. Katika mwaka wa fedha 2022/23, Serikali imetenga Shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati 300.

Amesema Jimbo la kalenga lina jumla ya zahanati 36 na kati ya hizo, zahanati 11 zinatoa huduma za maabara na zahanati 25 zinatoa huduma za maabara za msingi, Ili kuboresha huduma, serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za maabara katika zahanati.

Dk Dugange amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya afya kwa kujenga na kukarabati Vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi ya afya ya msingi.

Habari Zifananazo

Back to top button