Watumishi wamsikitisha RC Katavi uwekezaji la Luhafwe

KATAVI; Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesikitishwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kujihusisha na uchochezi wa migogoro katika eneo lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji la Luhafwe, lenye ukubwa wa hekta 46,000.

Hali hiyo imejitokeza baada ya RC Mrindoko akiambatana na Kamati Ulinzi na Usalama Mkoa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Idd Kimanta kufanya ziara ya kutembelea eneo hilo na kukutana na taarifa ya eneo moja kumilikishwa kwa wawekezaji zaidi ya mmoja.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amemwambia RC Mrindoko kuwa katika eneo hilo, halmashauri imepokea fedha kutoka kwa kampuni mbili ambazo ni Seedland na Meru Agro kitendo ambacho kinaleta ugumu kwa eneo hilo kuendelezwa.

Kufuatia hatua hiyo RC Mrindoko amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaaban Juma kufika ofisini kwake Novemba 20 akiwa na nyaraka zinazoonesha ramani ya eneo la Luhafwe na mikataba yote ya uwekezaji waliyoingia na wawekezaji, ikiwemo kiasi cha fedha halmashauri ilizolipwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya RC Mrindoko, imeeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Septemba 2023 imefanya shughuli ya upimaji na mpaka sasa wawekezaji wakubwa waliotajwa kupewa mashamba ni MPM (Mufindi Paper Mills), Seed Land, Mero Agro na ASA.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x