Watumishi wawili hospitali ya Babati kuchunguzwa
Watumishi wawili wa Hospitali ya Babati mkoani Manyara, wanachunguzwa kwa tuhuma za kumuacha mjamzito ajifungue mwenyewe na wao wakiendelea kula.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(Tamisemi) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeeleza kuwa inafanyia kazi tuhuma hizo kubaini kama kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma na kitaaluma na ikibainika hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni na sheria.
“Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendelea kuwakumbusha Wataalamu katika vituo vya kutolea huduma nchini kote kuwa wazingatie miongozo na taratibu za kitaaluma zilizowekwa na Serikali wakati wote wanapohudumia.” imeeleza taarifa hiyo.
–
Ofisi ya Rais TAMISEMI imeeleza kuwa imeona tuhuma hizo ambapo Sophia Bakari mkazi wa Mlombo katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, kujifungua wodini kwa kusaidiwa na Dada yake, baada ya wauguzi hao kuwasubirisha kwa madai kuwa alipaswa kula kwanza ndipo watoe huduma.