Wauguzi wafundwa kukabiliana na changamoto

WAUGUZI wametakiwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo kwa kufanya kazi kwa uaminifu, weledi na ushirikiano  mkubwa ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Dunani Mei 30, wauguzi waliainisha changamoto zao ikiwemo kutolewa lugha chafu na wagonjwa na pia kuhudumia wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.

Advertisement

Maadhimisho hayo yamefanyika leo  jijini Dar es Salaam katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) yakilenga kupongezana na kukubushana wajibu wao.

Akizungumza na wauguzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk Respisius Boniface amesema licha ya kuboreshwa kwa huduma za afya pia huduma kwa wagonjwa inatakiwa kuboreshwa.

“Tuko hapa ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya Wauguzi Duniani Tawi la MOI ikiwa ni hatua ya kupongezana mafanikio yaliyopatikana katika kada ya uuguzi ,kukumbusha maadili ya kazi  na kukukumbusha kutoa huduma bora za kiuuguzi ,”ameeleza.

Ameongeza kuwa lengo kubwa ni kuboresha huduma za afya kama serikali inavyotaka kwasababu serikali imewekeza sana katika miundombinu ya afya na miundo mbinu peke yake haitoshi tunasisitizwa sisi watumishi kutoa  huduma bora.

Dk Boniface amesema Katika tiba wauguzi ni kundi kubwa sana la watumishi wa tiba kwa asilimia 60 mchango wao ni mkubwa hivyo  wanasisitiza huduma bora.

Amefanua kuwa Changamoto iliyopo ni upungufu wa wauguzi ambapo MOI  wamekuwa wakiomba vibali vya ajira na serikali imekuwa ikiwapa  vibali vya ajira  na wa mekuwa wakiajiri kwa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani hivyo wanajitahidi kukabiliana na uhaba huo.

“Changamoto nyingine ni wagonjwa wanawajibu vibaya,wanatoa lugha zisizoelewaka kwanza tumewaelekeza kutoa huduma mzuri kwani wanapopata huduma nzuri hawatakuwa na majibu mabaya na tumekubaliana kuwa huduma za uuguzi ziwe nzuri kama watakuwa wanakwazwa na wagonjwa kikubwa waripoti.

Amesema kwa MOI muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 10  lakini kwa viwango vya kimataifa muuguzi mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa watatu na ICU mgonjwa mmoja na muuguzi mmoja.

Aidha amesema Idadi ya wauguzi MOI  ni 279 lakini mahitaji ili kazi ziende vizuri angalau wauguzi 500 ndio wanahitajika ambapo 2024  wameomba ajira ya wauguzi 60 serikali  na wengine 50 watawaongeza kwa mapato ya ndani.