Waumini waomba kituo cha yatima kisiuzwe

WAUMINI wa Msikiti wa Ijumaa wameiomba Serikali iwasaidie kuzuia uuzaji wa kituo cha kulea watoto yatima cha Islamic Yatima Foundation kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Maombi hayo yameombwa leo na mwakilishi wa waumini wa huo,  Masoud Mgasa wakati wa mahojiano maalumu na HabariLEO.

Mgasa amesema kituo hicho kisiuzwe kwani kimekuwa msaada mkubwa kwa watoto yatima kutoka Mwanza na mikoa mbali ya Kanda ya Ziwa.

Alisema kituo hicho kinatarajiwa kuuzwa baada ya aliyekuwa msimamizi wake (Sherally Hussein) kushinda kesi namba nne ya mwaka 2022 mahakamani.

Alisema pia kituo hicho kinatakiwa kumlipa fidia ya Sh milioni 78 kama sehemu ya stahiki zake pamoja na Sh milioni 31 kama gharama alizotumia kuendesha kesi hiyo ya madai ya malimbikizo ya mshahara.

Mgasa amesema hatua za kuuza kituo hicho kimetokana baada ya Sherally Hussein ambaye aliekuwa msimamizi wa kituo hicho kushinda kesi ya madai hukumu yake ambayo inatarajiwa kukaziwa Juni 7 mwaka huu.

Alisema endapo Hussein akishinda kesi hiyo itatakiwa kituo hicho kiuzwe.

‘’Tunatoa wito kwa waislamu na jamii kwa ujumla kuungana kwa pamoja na kuweza kuwasaidia watoto yatima wa Ilemela Islamic Yatima Foundation waendelee kupata huduma za malezi na Elimu kupitia kituo bila kuuzwa’’ amesema.

Amesema kituo hicho kina watoto 250 na watoto hao wamekuwa wakitegemea misaada mbalimbali kutoka kwa waumini wa msikiti huo pamoja na wadau mbali mbali.

Naye muumini mwingine wa msikiti wa Ijumaa Ramadhani Ally amesema kituo hicho kinahudumia watoto wengi yatima. Amesema anaiomba sana Serikali iweze kuwapigana na kuwasaidia kituo hicho kisiuzwe.

 

Habari Zifananazo

Back to top button