Wavamizi maeneo ya hifadhi waonywa Geita

SERIKALI wilayani Geita mkoani hapa, imetoa onyo kali kwa wananchi wanaoendelea kukiuka kanuni na sheria za mazingira kwa kuendesha shughuli binafsi ndani ya maeneo ya hifadhi na kuwataka kuondoka mara moja.

Onyo hilo limetolewa na Mshauri wa Jeshi la Akiba mkoani Geita, Kanali Johnson Kikoti kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, katika hotuba yake aliyoisoma wakati akihitimisha mazoezi ya kijeshi ya Timua Vumbi.

online pharmacy oseltamivir no prescription with best prices today in the USA

Mazoezi hayo ya kijeshi yamefanyika ndani ya hifadhi ya Msitu wa Geita eneo la Samina wilayani Geita, ili kuwajengea uwezo askari wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Akiba kwa uratibu wa kikosi cha JWTZ 23, Biharamulo, Kagera.

online pharmacy tobradex no prescription with best prices today in the USA

Kanali Kikoti amesema wananchi wanapaswa kupisha na kuheshimu Hifadhi ya Msitu wa Geita, ili kutunza misitu ya asili, kwani wakati mwingine hutumiwa na askari wa JWTZ kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuwajengea utimamu.

“Ni marufuku kufanya shughuli zozote za kibinafsi kwenye eneo hili, hii kazi mliyoiona leo ni endelevu, na hatutoa taarifa tena.

online pharmacy rogaine no prescription with best prices today in the USA

Mifugo na watu  ni marufuku, hakuna kukata mkaa, wala magogo, wala kuchoma moto.

“Kwanza uharibifu unatuharibia sisi wanajeshi kuweza kupata maeneo ya kujificha kufanyia shughuli zetu, pia sisi wenyewe kupata maeneo ya kufanyia mazoezi, pili tunahatarisha maisha ya vizazi vijavyo na mvua haitanyesha.”

Kamanda wa Kikosi cha JWTZ 23 Biharamulo-Kagera, Meja Raphael Paschal, amesema zoezi la timua vumbi limefanyika kwa muda wa wiki mbili kulenga kujenga utimamu, kuangalia uwezo wa dhana na uwezo wa kumudu vikundi.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Geita, Almas Mggalu amebainisha zaidi ya asilimia 50 ya eneo la hifadhi ya msitu wa Geita ambao una ukubwa wa hekta 50,800 limeharibiwa kwa shughuli za binadamu.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button