Wavamizi wa ardhi Bagamoyo waonywa

BAADHI ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa serikali katika Halmashauri ya Bagamoyo, mkoani Pwani wameonywa kuacha tabia ya kuvamia maeneo ya ardhi jambo ambalo limekuwa likichangia migogoro

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Bagamoyo, Abdusharifu Zahoro, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM wa kata za Yombo na Magomeni, wilayani hapa wakati wa ziara ya mbio za mbendera ya CCM.

Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakivamia maeneo na kuuza ardhi hizo mara mbili kwa wawekezaji hali ambayo imekuwa ikisababisha kuzuka Kwa migogoro ya ardhi isiyo kwisha.

“Kumezuka tabia ya baadhi yenu viongozi wa kata na vijiji kuvamia ardhi na kuziuza kwa matajiri na mnauza mara mbili nakemea tabia hii kwani imekuwa ikichangiwa kuongezeka kwa migogoro ya ardhi jambo hili halina Afya kwa Chama na Serikali”alisema

“Jambo hili linatutia aibu sana sisi viongozi wa chama na Serikali tunapaswa kubadilika na kuacha mazoea tumuunge mkono Mkuu wetu wa wilaya katika harakati za kukomesha migogoro ya ardhi ndani ya wilaya yetu hii”alisema

Alisema wananchi wamewapa dhamani viongozi hao kuwaongoza na kwamba wajibu wao ni kuhakikisha wanapigania maslahi ya serikali na chama kwa kufanyakazi Kwa uaminifu na uadilifu kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Katibu wa Chama wa wilaya hiyo, Yusuph Abdallah, aliwataka viongozi wa chama hicho kufanya vikao Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za cha ikiwa ni pamoja na kufanya siasa shirikishi sambamba na kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuimariaha uchumi.

Diwani wa kata ya Yombo, Mohamed Husinga, alisema katika kipindi cha miezi mitatu serikali imetoa zaidi ya milioni 300 Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, nyumba za walimu na matundu ya vyoo.

Habari Zifananazo

Back to top button