WENZA, Vaileth Kawovela na Evodius na Gozbelt wakazi wa Kibaha, mkoani Pwani wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wanaonufaika na huduma za matunzo kupitia Taasisi Tanzania Health Promotion Support (THPS) wanatarajia kufunga ndoa mwaka 2024.
Wamesema hayo walipozungumza na gazeti hili kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Disemba mosi mwaka huu ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro.
Wenza watarajiwa hao waliishukuru Taasisi THPS inayosimamia mradi wa Kituo cha Kimarekani cha Kudhibiti Magonjwa ( CDC) chini ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI, (PEPFAR) na Afya hatua kwa kuweza kuwafikisha hapo walipofikia.
Kawovela ambaye ni mama mtarajiwa alisema , THPS imeweza kumlea yeye kuanzia akiwa mtoto hadi sasa akwia amefikisha umri wa miaka 24 baada ya kuzaliwa na maambukizi hayo , na kupatiwa huduma rafiki tangi akiwa mtoto .
‘ Hatua hii iliendelea kunipa furaha na kufarijika kwani Taasisi hii imeweza kunileta tangu nikiwa na umri mdogo hadi sasa nimefikisha umri wa miaka 24 “ alissema Kawovela .
Kawovela alisema THPS ilikuwa inatoa huduma rafiki kuanzia alipokuwa na umri ndogo alipokuwa akifikishwa kwenye kituo cha Afya kwa ajili ya kliniki ya kupata dawa huku akichanganywa kucheza na watoto wengine.
“ Tulikuwa tunacheza na watoto wenzetu na wao walikuwa wanatusukuma kwenye bembea na wanatugawia pipi na maziwa”, ilinipa furaha kwa vile tunakutana na watoto wengine huku wao wakituhumiza sisi ( watoto) tusiachekunywa dawa ili tuwe na afya nzuri “ alisisitiza Kawovela.
Kawovela alisema, wakati mwingine watumishi hao walitumia mbinu za kuchukua mfano wa dawa sijui ni za kutuliza maumivu na kuzimeza mbele ya watoto na kitendo hicho kilikuwa kuonesha hakuna madhara yoyote.
Alisema kitendo hicho kiliwahamasisha wao ( watoto) kujenga shauku ya kupenda kwenda Kituo cha Afya kila mwisho wa mwezi kukutana na watoto wenzao ili wapatiwe maziwa na pipi.
Alisema ,tangu kipindi hicho ameendelea kunufaika na huduma rafiki kwa vijana ambazo zimeendelea kumsaidia kukua kiakili , kujitambua na kuchangamana na vijana vituo vingine na kuona ya kwamba hayupo pekee yake.
Kawovela alisema ,kupitia mradi huo ulianzisha klabu zao na pia kupitia klabu za vijana chini ya mradi huo zimemwezesha kukutana na mwenza wake , kuendelea kutambuana zaidi na hatimaye kuwa na mahusiano ( mapenzi) .
“ Mpaka sasa hivi tunatarajia kufunga ndoa mwakani Mungu akipenda na pia tunatarajia kupata mtoto siku za karibuni “ alisema Kawovela .
Alisema anamshukuru Mungu kwa sasa yenye ni mama mtarajiwa ambapo anaendelea kupata mafundisho na elimu ili niweza kumzaa mtoto wangu akiwa salama.
“… japo kuwa hata sasa yapo maelekezo ambayo ninapewa ili niweze kuzaa mtoto salama ambaye hatakuwa na maambukizi” alisema Kawovela
Anasema mafundisho na elimu anayopewa ni kwa ajili ya kupewa tahadhari kuhusu mkumkinga mtoto na maambukizi wakati wa ujauzito , kuzaliwa na wakati wa kunyoyesha .
“ Wakati wa ujauzito ukipata haya mafunzo ndipo tunazungumzia mtoto amezaliwa …jambo kubwa unapewa tahadhari dawa za kinga ambazo anapewa mtoto asije akapata maambukizi wakati wa kumyonyesha “ alisema Kawovela .
“…anazitumia hizo dawa na baada ya miezi kadhaa anapimwa afya yake , mara ya kwanza , ya pili nay a tatu na kuthibitishwa kama hanaa maambukizi basi anaendelea na maisha yake “ alisema Kawovela .
Kwa upande mume mtarajiwa wa Kawovela, Evodius Gozbelt, ambaye ni mkazi wa mkoa wa Pwani , anashukuru ufadhili uliotolewa na kuendelea , umewatoa sehemu moja na kuwafikisha sehemu salama.
Alisema kwake kutokana misaada hiyo na klabu zinazosimamiwa na Taasisi hiyo imemwezesha kupata mchumba ambaye anatarajia kufunga naye ndoa mapema mwakani (2024) ingawa kwa sasa ni wakati wowote anatarajia kujifungua mtoto.