Wavutiwa upigaji hatua kiuchumi, uhifadhi

TIMU ya wataalam kutoka Benki ya Dunia inayoendelea na kazi yake ya kutathmini utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), umevutiwa na namna vikundi vya kijamii vinavyowezeshwa na mradi wa REGROW kiuchumi, kwa namna vinavyopiga hatua ya kimaendeleo kiuchumi na kiuhifadhi wa maliasili nchini.

Akizungumza kwenye ziara ya wataalam hao, katika kijiji cha Kisaki Kituoni, Mratibu Msaidi wa Mradi wa REGROW kutoka Benki ya Dunia Nicholas Soikan licha ya kuvipongeza vikundi hivyo, amesema lengo la Benki ya Dunia kuipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu kutekeleza mradi huo, ni kuona watanzania wananufaika na urithi adhimu wa maliasili zilizopo hususani Kusini mwa Tanzania, kwa kuboresha usimamizi wa maliasili hizo, kukuza Utalii na kuwainua wanachi kiuchumi.

Soikan ameongeza kuwa nifaraja kubwa kuona na kuwasikia wananchi wakitoa ushuhuda wa namna mradi wa REGROW ulivyoweza kubadili maisha yao kiuchumi na kimtazamo wa umuhimu wa Hifadhi ya Taifa Nyerere katika maendeleo ya nchi kwa ujumla, jambo linalo pelekea Wanakijiji hao kuwa sehemu ya Uhifadhi endelevu wa Hifadhi hiyo kubwa kuliko zote Duniani.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanakijiji cha Kisaki Kituoni, Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Shabani Mgohamwelu, ameeleza kuwa mradi wa REGROW umewapatia furaha wananchi na kuwa wanakijiji hicho wataendelea kuwa sehemu ya Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Nyerere kwa kuwa wameona manufaa makubwa ya kuishi jirani na Hifadhi hiyo, huku akiwaomba Wataalam hao kutoka Benki ya Dunia kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali  ya kuwaletea watanzania maendeleo.

Aidha kupitia mradi wa REGROW, hadi sasa katika Kijiji cha Kisaki Kituoni vikundi 12 vyenye jumla ya wanachama 222 vimepatiwa fedha mbegu sh milioni 120,930,200 na fedha kwa ajili ya miradi sh 234,517,301.20 huku wanafunzi 35 wakipatiwa ufadhili wa masomo.

Katika hatua nyingine timu ya wataalam hao kutoka Benki ya Dunia wakiwa wameambatana na Watekelezaji wa Mradi wa REGROW nchini, wametembelea na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Hifadhi ya Taifa Nyerere ukiwemo uwanja wa ndege wa Mtemere.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button