WAVUVI kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, Simiyu, Mwanza, Geita, Mara na Kagera wametakiwa kuacha mgomo na kurejea katika masoko yao ili kuendelea na biashara zao.
Rai hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Agnes Meena alipozungumza na wafanyabiashara hao kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa katika ukumbi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Meena amewahidi wafanyabiashara hao serikali itafanyia mapendekezo mbalimbali wafanyabiashara hao waliopendekeza ikiwemo kupunguzwa tozo.
Amesema pendekezo jingine liliotolewa na kuwe na ushirikishwaji wa wavuvi pamoja na wafanybiashara wa samaki katika kupanga tozo.
Amewahidi wafanyabiashara hao ndani ya wiki moja maombi yao yatafanyiwa kazi na watapewa mrejesho.
Amewaomba wafanyabiashara hao kurejea katika masoko yao na kuendelea katika biashara zao huku akiwaomba wasigome.
Naye katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya amesema maoni ya wafanyabiashara wa samaki yamechukuliwa na amewaomba wafanyabiashara hao kuwa na subira na kuendelea na kazi zao.
Mfanyabiasha wa dagaa kutoka kisiwa cha Mazinga Mkoa wa Kagera, Deogratius Biseko amesema chanzo kikubwa cha mgomo wao ni kuongezeka kwa tozo za ushuru.
Amesema ana imani na serikali itafanyia utatuzi wa hoja zao na kuweza kuwasaidia kupata muafaka ili waweze kurejea katika masoko na kufanya biashara zao.
Ameiomba serikali iendelee kuwatafutia masoko ya samaki katika nchi mbali mbali.ili waweze kufikisha bidhaa za samaki.