Wavuvi Kivu washtushwa na uhaba wa samaki

JAMII ya wavuvi katika Ziwa Kivu wamesema upatikanaji wa samaki katika ziwa hilo umeshuka na kuathiri uchumi wa wananchi wa Kivu wanaotegemea uvuvi wa samaki kama chakula na kipato cha kukuza uchumi wao.

Mratibu wa Mradi wa Uvuvi wa Kibuye, Jean-Bosco Sibomana ambaye anaratibu uvuvi wa samaki katika wilaya za Karongo, Rutsiro na Nyamaseke alisema kiwango cha samaki kinachopatikana sasa hivi ni kidogo ikilinganishwa na mwaka 2020.

Alisema wakati wa kiangazi wavuvi wanapata samaki kuanzia kilo 20 hadi 40 kwa siku za mavuno mazuri na kilo 10 hadi 15 katika kipindi chenye uhaba wa samaki wakati mwaka jana kipindi kama hicho walikuwa wanapata kuanzia kilo 60 hadi 70 za samaki.

Kupungua kwa mazao ya samaki katika eneo la Kivu kumesababisha kushuka kwa soko la samaki na kuathiri kipato cha wananchi.

Serikali ya Rwanda imeahidi kushughulikia suala la upungufu wa samaki kwa watu wa Kivu na kujua tatizo la ukosefu wa samaki linasababishwa na nini.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x