Wavuvi wawili wafa maji Ziwa Victoria

WAVUVI wawili katika mwalo wa Bunyorwa, kandokando ya Ziwa Victoria, Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu wamefariki dunia, baada ya kuzama katika ziwa hilo wakiwa wanavua samaki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Bladius Chatanda, imewataja wavuvi hao kuwa ni Ntambi  Swilila (32) mkazi wa kijiji cha Kahangalala Wilaya ya Busega na Deus Ntandila (56), mkazi wa kijiji cha Mwanegeyi Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Taarifa imesemoa tukio hilo lilitokea Septemba 18 mwaka huu, majira ya saa 8 usiku, wakiendelea na shughuli zao za uvuvi, huku manusura wa ajali hiyo ni Isacka Masigani (20),  mkazi wa Kijiji cha Kitongo Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza na Sahani Simba (21), mkazi wa kijiji cha Masanza wilaya ya Busega, waliokolewa na wavuvi wenzao waliofika eneo la tukio kutoa msaada.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya mtumbwi wao kusukumwa na upepo mkali na kuzama na kwamba miili ilionekana juzi Septemba 20, 2022.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x