TIC kuweka mazingira safi uwekezaji

SERIKALI kupitia Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) imeeleza kuwa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa Kitanzania ili kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na kituo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri amesema hayo alipowatembelea baadhi ya wawekezaji wa Kitanzania jijini Mwanza kwa lengo la  kuwahamasisha wawekezaji wa ndani kufanya uwekezaji huku akiongeza kuwa taasisi hiyo inafanya uhamasishaji wa uwekezaji ili Watanzania waweze kujikita kwenye kuwekeza mitaji yao.

“Hapo awali ulikuwa ukisema neno uwekezaji kitu cha kwanza kinachomuijia mtu kichwani mwake ni wageni wanapaswa kuwekeza lakini sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022 imepanua wigo kuhakikisha Watanzania wana nafasi mara kumi zaidi kuwa wanufaika na vivutio vya uwekezaji na kuweza kuwafikia kiurahisi zaidi katika kuwekeza nchini kwao ukilinganisha na wageni”.Amesema

Mkurugenzi wa Kampuni ya Chobo Investment ya jijini Mwanza inayojihusisha na uchakataji na usindikaji wa nyama, John Chobo amesema kuwa  lengo la kuwekeza katika kiwanda hicho ni kuhakikisha wanakizi mahitaji ya ndani ya  nchi ili wasitegemee nje ya nchi.

“Masoko ya huko nje yanahitaji nyama za kutosheleza ndio maana tuna mashamba ili kuongezea uandaaji wa mifugo ambayo itakuwa sahihi kwa mlaji ili kuweza kukizi kiwango kinachopungua”. Alisema Chobo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amesema  Serikali imewekeza fedha kwa ajili ya ufugaji wa samaki wa kisasa katika Ziwa Victoria ili kuhakikisha viwanda vinafufuliwa ili kuchakata minofu mingi ya samaki Kwa ajili ya kusafirisha.

“Kwa hiyo nyie kituo Cha uwekezaji Tanzania TIC kuja Mwanza ni fursa Kwa wawekezaji wa ndani kuelewa serikali imeimalisha mifumo ya taarifa ya sheria ya uwekezaji pamoja kuboresha mazingira ya kupata leseni Kwa muda mchache”. amesema Makalla”

Makalla ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza ni wakimkakati kutokana wa pili kuchangia pato la taifa Kwa asilimia 7.15 ukiongozwa na Dar- es- salaam, juhudi katika uwekezaji unahitajika kupitia sekta mbalimbali za hapa.

” Kwa hiyo mimi nisema kuwa kituo cha uwekezaji Tanzania bora mmekuwa na ofisini inayotembea Kuna watanzania wenye fedha lakini hawafahamu kuwa wanapaswa kusaidiwa na nyie TIC kutoka kwenu kuja huku kitawasaidia Watanzania kuelewa vigezo vya mtu kuwa mwekezaji”. Alisema Makalla.

Habari Zifananazo

Back to top button