Wawekezaji waitwa hifadhi ya Pindiro

WAWEKEZAJI kutoka ndani na nje ya nchi wamealikwa kuwekeza katika hifadhi ya msitu asilia wa Pindiro ulioko Kilwa kwa kujenga hoteli za kitalii na vivutio vingine.

Wito huo umetolewa na ofisa utalii kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Wilaya ya Kilwa, Nurdin Omari alipozungumza na HabariLEO.

Nurdin alisema jana kwamba zaidi ya ekari 20 zimetengwa katika msitu huo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kitalii, kambi na nyumba za kulala watalii.

Nurdin alibainisha kuwa sheria na taratibu za jinsi ya kuwekeza katika hifadhi ziko wazi, hivyo ni nafasi kwao kuwekeza katika hifadhi hiyo.

Alisema katika hifadhi hiyo kuna vivutio mbalimbali kama vile viboko albino ambao hawapatikani sehemu nyingine, mamba, nyoka na miti ya asili.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button