Wawekezaji waitwa Katavi

WAWEKEZAJI nchini wameombwa kuendelea kuwekeza katika Wilaya ya Tanganyika na Mkoa wa Katavi kwa ujumla kwa kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha miundombinu rafiki inapatikana, ili kurahisisha mzunguko wa kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi , Martha Mariki wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea kata za mkoa wa Katavi alipofika katika Kata ya Bulamata na kutembelea kiwanda kidogo cha kuchakata mafuta ya alizeti.

“TumieniĀ  fursa hii kuwakaribisha wawekezaji katika wilaya ya Tanganyika na mkoa wetu wa Katavi, mwekezaji huyu ameona inafaa kuanzisha kiwanda hiki kidogo na kutoa fursa ya ajira kwa vijana,” amesema Martha.

Amesema serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha umeme unafika katika Kata hiyo, ili kurahisisha mzunguko wa kiuchumi unaotegemea nishati ya umeme.

“Tunaona nguzo za TANESCO zinasimikwa hapa muda si mrefu umeme utawashwa kwenye kata hii na kurahisisha kazi za kiwanda hiki,” amesema.

Katika ziara hiyo Mbunge huyo ametoa Sh 500,000 kwa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Kata ya Bulamata , ili kuwainua kiuchumi.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button