Wawekezaji waitwa kurudisha Tanga ya viwanda

Wawekezaji waitwa kurudisha Tanga ya viwanda

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imetenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 5635, kwa àjili ya uwekezaji sekta mbalimbali ili kurudisha Tanga ya viwanda.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji hilo Dk Spora Liana, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, kuhusu walivyojipanga fursa za uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yana miundombinu yote rafiki na yanaweza kufikika kwa urahisi na yapo kwenye maeneo ya kimkakati kwa ajili ya kuendeleza uchumi.

Advertisement

“Tumedhamiria kuirudisha Tanga ya viwanda, hivyo tunawaita wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali niwahakikishie hakuna urasimu na maeneo yote yamepimwa,”amesema Mkurungenzi huyo.

Amesema historia inaonesha kuwa zamani Jiji la Tanga, lilikuwa na viwanda vingi, lakini vimekufa, hivyo wamedhamiria kuifufua Tanga ya zamani, ili kufungua fursa ya ajira na kipato kwa wananchi.