Wawili familia moja wafa kwa kutumbukia kisimani

MOROGORO; WATOTO wawili wa familia moja wamefariki dunia baada ya kutumbukia na kuzama kwenye Kisima cha maji kilichokuwa karibu na makazi yao kwenye Kijiji cha Lukonde, Kata ya Tomondo ,Wilaya ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha leo Machi 29, 2024 kutokea kwa tukio la watoto hao wawili kufariki dunia baada ya kutumbukia kisimani.

Watoto hao ni Godfrey Francis mwenye umri miaka mitano mwanafunzi darasa la awali  katika Shule ya Msingi Lukonde na Deus Ignas Kavishe mwenye umri wa miaka mitatu, wote watoto wa Anitha Zacharia Ndile.

“ Ni kweli watoto wawili wamefariki dunia kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji karibu na eneo la makazi yao walikuwa wakichota maji kwenye hicho, walizidiwa na utelezi wakatumbukia ndani ya kisima hicho cha maji, “ amesema Mkama.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Lukonde, Kata ya Tomondo, Wilaya ya Morogoro, Pius Pius amezungumza kwa njia ya simu na HabariLEO na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28, 2024 majira ya saa saba mchana.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button