Wawili mbaroni uingizaji vifaa vya intaneti

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao wamewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi wa Kawe, Kinondoni na Hongliang Yang (35) raia wa China , mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Watuhumiwa hao inadaiwa wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya intaneti nchini kupitia mtandao ya kijamii wa instagram kwa akaunti yenye jina la Starlink.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo,  Jumanne Muliro amesema baadhi ya vifaa hivyo vimeshauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam, kitendo ambacho ni kosa na  kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ametaja vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12 na Starlink Router 12, hivyo kutoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.

 

Habari Zifananazo

Back to top button