Wawili wafa ajali iliyoteketeza mabasi

RUVU, Pwani: KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa ikiwemo askari wawili wa jeshi la zima moto na uokoaji katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria kugonga gari la mafuta.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo eneo la Ruvu mkoani Pwani, ikihusisha gari ya Kampuni ya Sauli na New Force pamoja na lori la mafuta.

Kamanda amewataja waliojeruhiwa ni Koplo Hamisi kubwi na Koplo Elias Bwire, ambao walikimbizwa Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam na hali zao zinaendelea vizuri.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva wa mabasi yote mawili kushindwa kuchukua tahadhari.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button