Watu sita wafa kwa radi Mtwara

WATU sita wamekufa na wengine tano kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa kwenye sherehe ya kumpongeza kijana wao aliyehitumu kidato cha nne.

Tukio hilo limetokea jana katika kijiji cha maparagwe kata ya Chikukwa wilayani Masasi, mkoani wa Mtwara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo ametoa taarifa hiyo leo Disemba 2, 2023 na kusema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 jioni.

Amewataja waliofariki kuwa ni Patrick Maurus (42), Fatuma Rashid (40), Rosina Wales (46), Regina Vincent (55), Zainab Abdulrahaman (62) na Zainabu Mussa (44).

Habari Zifananazo

Back to top button