GEITA: Watu wawili wamefariki dunia huku wengine 28 wakinusurika baada ya watu 30 waliovamia eneo la mgodi uliozuiliwa kijiji cha Kanegere wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya kufunikwa na kifusi.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo na kueleza ajali hiyo ilitokea Septemba 10, 2023.
Kamanda Jongo amewataja waliofariki ni mkazi wa mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, Justine Godwin (23) pamoja na mkazi wa wilayani Bariadi mkoani Shinyanga anahefahamika kwa jina la Wilson Masunga (23).
“Mgodi huu ulikuwa umefungwa na watu walikuwa wamezuiliwa kuingia kwenye mgodi huo. Hao watu ni maarufu kama manyani, walipita njia za panya na kuvamia ule mgodi kuanza kuchimba.
Ameesha, wananchi wasamaria wema walianza juhudi za uokoaji baada ya kupata taarifa na kufanikiwa kumuokoa Justine akiwa hai na kueleza kuna wenzake wengi shimoni lakini naye alikuja kufariki baadaye.
“Juhudi za uokoaji zilifanyika na wale watu wote waliokolewa na kubaki mtu mmoja, na mpaka tarehe 13 (Septemba) ndipo mtu huyo aitwaye Wilson Masunga (23) mkazi wa bariadi mwili wake ulipopatikana.
“Naomba tu nitoe wito kwa wachimbaji wadogo, pale ambapo serikali ama watalaamu wanaposema kwamba eneo hili ni hatarishi na halifai kwa uchimbaji tuache kuchimba haraka iwezekanavyo.
“Lakini unapojifanya wewe ni mzoefu na una hakimiliki za kuchimba, mvua huku zimeanza kunyesha, tunapata maafa kwa sababu wachimbaji wanakiuka kanuni.
Kamanda ameeleza lipo tatizo kubwa la wachimbaji wadogo kutumia njia za panya kufika maeneo ya migodi iliyozuiliwa na hatimaye kupelekea majanga kwa watu kupoteza maisha kwa kufukiwa migodini.
Comments are closed.