Ajali: Wawili wahofiwa kufa makutano Musoma, Tarime

WATU wawili wanadaiwa kufa baada ya gari walilopanda kufeli breki, kuacha barabara na kuingia mtaroni kisha kulipuka katika makutano ya barabara itokayo Musoma-Tarime kuelekea Mwanza na mkoani Mara.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema gari namba T828 BEJ, liliangushwa na tela.

“Hatujafahamu idadi ya watu waliokuwa katika gari hili tofauti maneno ya mashuhuda wanavyosimulia pia bado tunafanya jitihada kuona kama bado wapo hai au wamekufa. kulikuwa na watu wangapi. “alisema Magere.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara,  Salum Morcase amesema gari hilo lilikuwa linatoka Mwanza na kwamba hadi sasa haijajulikana lilipokuwa likielekea.

“Nimeona gari linakuja kwa kasi sana likaingia mtoni ndani ya sekunde mbili likalipuka na hakuna mtu aliyeweza kutoka kwenye gari,” amesema Zaida Makasi.

Habari Zifananazo

Back to top button