Wawili wanaswa mauaji ya Kiplagat

POLISI nchini Kenya wamewakamata watu wawili waohusishwa na mauaji ya mwanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat.

Wanaume hao wawili wanaoaminika kuwa na umri wa miaka 30 walikamatwa eneo la mji wa Eldoret.

Kiplagat ameiwakilisha Uganda katika michezo mitatu ya Olimpiki na kushiriki katika michuano sita ya dunia. Mafanikio yake mashuhuri ni pamoja na kufika nusu fainali ya Olimpiki ya London 2012 katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi.

Advertisement

Mwili wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 ulipatikana kwenye gari Jumamosi usiku ukiwa na jeraha kubwa la kisu shingoni.