Wawili wapigwa risasi, mechi ya Sweden, Ubelgiji ikisimamishwa
MCHEZO wa kufuzu michuano ya Euro, kati ya Ubelgiji na Sweden umesimamishwa huku wachezaji wakikataa kujitokeza kipindi cha pili.
Haya yanajiri baada ya mashabiki wawili wa soka wa Sweden kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Brussels kabla ya mchezo huo usiku wa leo.
Matokeo yalikuwa 1-1 wakati wa mapumziko hata hivyo uamuzi ulipochukuliwa wa kusimamisha mchezo na mashabiki waliambiwa kubaki kwenye Uwanja wa King Baudouin “hadi usalama utakapowaruhusu kuondoka.”
Tangazo katika uwanja huo lilisema: “Wachezaji waliamua kutotaka kuendelea na mchezo, kwa sababu ya kile kilichotokea mapema leo huko Brussels.”
Kauli hiyo ilitolewa kwa Kiingereza, Kifaransa, Kiholanzi na Kiswidi na umati ulipiga makofi baada ya tangazo hilo.