Wawili wapoteza maisha ajali ya gari Kibaha

WATU wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na gari la mizigo kata ya Mkuza wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alisema ajali hiyo ilitokea Julai 26, 2023, majira ya 8:30 usiku barabara kuu ya Dar es Salaam/Morogoro.

Alisema watu hao wawili walifariki papopapo na wengine wa tatu kujeruhiwa baada ya gari yenye namba za usajili T370 DHA aina ya Higer Mali ya kampuni ya mabasi ya Saratoga likiendeshwa na Dereva Ammy Anuru, kugongana na gari lenye namba za usajili T. 925 DRH lenye tela namba T 560BLA aina ya Howo.

“Basi la abiria Saratonga lilikuwa likitolea mkoani Kigoma kuelekea Dar Es salam liligongana na gari hiyo ya mizigo ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salam kwenda Morogoro likiendeshwa na Dereva Hussein Hassan (37) na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo”alisema

Kamanda aliwataka waliofariki kuwa ni poja na Dereva wa basi Hilo la abirikkia Ammy Anuru (37) na kijana mwingine mwenye jinisia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25 ambaye jina lake hajijafahamika.

Aidha alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Saratonga kupita magari mengine bila kuchukua hatahadhari na kwamba waliojeruhiwa ni mnili Mohamed (36), Shabani Bomeka wote wakazi wa Kigoma Ujiji na Amani Jonathan mkazi wa Ilala Jijini Dar es salaam.

Kamanda alisema majeruhi hao wanapatiwa matibabu katika Hosptali ya Mkoa wa Tumbi na miili ya marehemu imehifadhi hosptalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na baadae itakabidhiwa Kwa ndugu zao Kwa ajili ya mazishii.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button