“Wazazi hakikisheni watoto wanafika shule”

MWANZA: WANAFUNZI 11,332 kutoka Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wanatarajia kujiunga na kidato cha Kwanza kwajili ya mwaka wa masomo 2024.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Shibula, Ofisa Elimu sekondari, Sylvester Mrimi amesema wanatarajia kupokea wavulana 5,502 na wasichana 5,830.

Amewaomba wazazi kuhakikisha wanafunzi wanafika shule kwa wakati ilikuanza masomo yao mara moja.

Kwa upande wake Ofisa elimu awali na msingi, Marco Isaka amesema kwa mwaka huu wanatarajia kuandikisha wanafunzi 13,800 wa awali na mpaka sasa ni asilimia 35 ndio waliohudhuria masomo na wanatarajia kuanzia Januari 12, 2024 na matarajio waliyonayo yatakuwa yamefikia lengo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Kiomoni Kibamba amesema atahakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na walioandikishwa shule za awali na msingi wanaudhuria shuleni.

Amewataka kuwahimiza watoto kufika shuleni ilikuanza masomo haraka iwezekanavyo.

“Serikali imeisha lipa ada zote za wanafunzi na miundo mbinu iko vizuri kwakuwa serikali imeishatimiza wajibu wake kwa kujenga madarasa,matundu ya vyoo,ofisi za walimu imeleta vitabu vya wanafunzi  hivyo nawahimiza wazazi walete watoto wao na wahakikishe watoto wao hawatoroki masomo ili wapate elimu’’ amesema .

Mmoja ya wazazi waliopelekea watoto wao shuleni,Stella Evaristi ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu watoto wasiokuwa na sare za shule kujiunga na masomo kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu kwa baadhi ya wazazi.

Amesema kuwa Rais Samia amesaidia kuboresha elimu kwa watoto hususani wa kike kwa kuwapa kipaumbele cha elimu mtoto wa kike anapopata elimu anaepukana na mimba za utotoni na ndoa katika umri mdogo.

Habari Zifananazo

Back to top button