“Wazazi msichapishe picha za watoto mitandaoni”

WAZAZI wameshauriwa kutochapisha picha za watoto wao mitandaoni ili kulinda haki zao.

Mkufunzi kutoka Jamii Forum, Francis Nyonzo alitoa ushauri huo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya usalama wa kidijitali yaliyotolewa kwa waandishi wa habari.

Advertisement

Badala ya kuweka picha za watoto, ameshauri kuweka matukio ya kijamii yanayoendana na shughuli zako za kila siku.

Kwa upande mwingine waandishi wameshauriwa kuzitambua haki zao za msingi katika ulinzi na usalama wa vifaa vya kazi kama vile simu na kompyuta.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), kwa kushiriiana na Jamii Forum.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *