“Wazazi msikwepe majukumu”

WAZAZI na walezi wametakiwa kutokukwepa majukumu ya malezi ya watoto kwa kuwapeleka sehemu za kutunza watoto au shule za bweni na badala yake wachukue jukumu la kuwalea wao wenyewe katika maadili mema.

Akizungumza katika mdahalo wa kujadili kuhusu momonyoko wa maadili hapa nchini ,Mratibu dawati la Jinsia wa Chuo cha Al-Maktoum iliyopo jijini Dar es Salaam ,Subira Nzole amesema lengo ni kuamsha ufahamu katika jumuiya ya wanafunzi na majirani wanaowazunguka.

Amesema kuwa wanataka jumuiya ifahamu juu ya momonyoko wa maadili na washiriki katika kujenga maadili badala ya kubomoa.

“Mdahalo huu unafanyika kwa mara ya kwanza tunafanya kama agizo la serikali tutafanya tena mbele ili kuamsha wanajuimaya kujua maadili ni nini ? wajue kuepuka maadili mabaya na kukaa na kuwalea watoto wao katika maadili mema,”amesisitiza Nzole.

Amewashauri vyuo vingine kufanya midahalo kama hiyo ili kuwajenge uwezo wanafunzi wao ambao ni wazazi wa kesho na kuamsha uelewa.

Amesema Vijana wanatakiwa kujua maadili ni kitu gani ?kama wazee wao walivyowalea waishi katika maadili mema na waepuke maadili mabaya ya uovu kama vile kuamua kutumia dawa za kulevya,kufanya vitendo vya wizi,kuuza miili na matendo mengi mabaya ambayo sasa yanaelendela dunia.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam , Veronika Mika ameeleza kuwa midahalo kama hiyo inaweza kuwasaidia wanafunzi na watu ambao wanazungukwa na chuo hicho kuweza kupunguza ukatili katika jamii na kuimarisha masuala ya maadili .

Amefafanua kuwa Serikali imekuwa ikitumia jitihada kubwa kupita katika shule na vyuo kuelimisha jamii pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali kuwafanya wasijiingize katika vitendo viovu.

“Kupitia midahalo kama hii tunategemea kupata jamii yenye kuzingatia maadili lakini pia niwasihi wazazi waweze kuungana serikali kwaajili ya kupinga momonyoko wa maadili kwa kuwajenga watoto kuanzi wakiwa wadogo tutakapoungana tutaweza kufanya jamii kuwa na maadili mema na kuondoa vitendo viovu,”amesistiza Ofisa huyo.

Naye mmoja wa Wanafunzi aliyeshiriki katika mdahalo huo ,Asma Hamad amesema Mdahalo huo utamsaidia kujua malezi ambayo atawapatia watoto kwani yeye ni mzazi mtarajiwa.

Amesema kuwa pia atatumia elimu hiyo kufundisha jamii ili iweze kuelewa na kutoa malezi yenye maadili mema.

“Tutaweza kuwalea watoto wetu kupitia haya tunayojifunza kulea kama nilivyolelewa au nitawapotosha kwani malezi ni chimbuko la momonyoko wa maadili.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x