Wazazi wa watoto ‘Njiti’ kuvaa mavazi maalumu

DAR ES SALAAM: WABUNIFU wa mavazi nchini wamebuni na kuonyesha mavazi 12 tofauti maalumu yatakayovaliwa na wazazi Mama au Baba wanaolea watoto njiti.

Vazi hilo ni maalum ambalo litamsaidia muhusika kumlea vizuri mtoto ambae amezaliwa kabla ya muda ‘ Njiti” akiwa hospitalini na hata baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitalini.

Advertisement

Ubunifu huo wa mavazi umeonyeshwa katika maonyesho makubwa ya Mavazi yanayojulikana kama “Swahili Fashion Week” yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika maonyesho hayo , Doris Mollel ambae taasisi yake inajihusisha na masuala ya watoto Njiti’ amesema taasisi hiyo iliwapa hamasa wabunifu kushona mavazi yao ili kuelimisha jamii kupitia makundi mbalimbali.

“Leo tumeifikia tasnia hii ya mitindo inayowagusa watu wengi wakiwemo vijana, mavazi tofauti tofauti yaliyoonyeshwa yanayoweza kutengenezwa na kusaidia wazazi wanaopata watoto njiti kuhudumia watoto wao kupitia huduma ya Kangaroo Mother Care (KMC) na sasa pia tuna Champion Baba afanye (Kangaroo Father Care – KFC), ” amesema.

15 comments

Comments are closed.