Wazazi wampongeza Samia kuruhusu mikutano ya siasa
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya amempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini.
Maganya amesema hayo leo jijini Arusha, wakati akitoa tamko la jumuiya hiyo kwa waandishi wa habari.
Amesema fursa ya mikutano ya hadhara iliyotolewa na Rais Samia ni kuonesha namna bora ya kuendesha siasa hapa nchini.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kumtia moyo Rais Samia, kwani umoja na mshikamano ndio msingi wa maendeleo katika nchi yetu,” alisema.