Wazazi watakiwa kuonesha upendo kwa watoto

WAZAZI wametakiwa kuwalea watoto tangu wakiwa tumboni ili kuwaonyesha upendo kabla hawajazaliwa.

Akizungumza jana mkoani Mtwara katika uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) Mkoa wa Mtwara, mtaalamu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka Shirika la Children in Crossfire, Davis Gisuka amesema upendo wa mtoto utahamia kwa mtu ambaye ataonyesha upendo na kuwa karibu naye.

‘’Wazazi tunapaswa tuanze kuwalea watoto si tu pale wanapozaliwa tangu wakiwa wako tumboni yaani mimba ikisha tunga ndipo tunatakiwa sasa kuanza kuandaa malezi ya mtoto kwahiyo baba na mama tuanze kuonyesha upendo kabla ya mtoto kuzaliwa.”amesema Gisuka

Aidha nyanja tano zinazomfanya mtoto aweze kukua kuanzia miaka 0 mpaka 8 ikiwemo lishe bora, ulinzi na usalama wa mtoto, afya, utunzaji wa awali, malezi yenye mwitikio ambazo zitamsaidia mtoto huyo kufikia utimiifu wake kwa kukua kiakili, kimwili, kijamii na kihisia.

Meneja mradi wa mtandao wa malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ya mtoto nchini (TECDEN), Lazaro Ernest amesema wameona kuwepo kwa baadhi ya changamoto zinazoikumba jamii mkoani humo ikiwemo lishe duni kwa watoto wa umri huo hivyo wanazichukulia kwa uzito mkubwa na bado wana kazi kubwa ya kufanya kama wadau kwa kushirikiana na serikali, kukabiliana na changamoto hizo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Salome Francis amesema progamu hiyo kama itatekelezwa vile inavyotarajiwa italeta matoekeo chanya kwa watoto wa umri huo kutokana imeenda mbali zaidi hiyo wanatakiiwa kuwezeka zaidi katika masuala ya malezi na makuzi kwa watoto.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema program hiyo ni chachu ya kuwakumbusha wadau wote wanaohusika na afua za watoto wenye umri huo kuhakikisha watoto hao wanapata huduma za malezi jumuishi ili waweze kufikia ukuaji timilifu.

Aidha ameutaka viongozi mbalimbali na wadau wote wanaotekeleza afua za watoto hao yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali kutekeleza shughuli zao kwa mujibu wa sheria, sera na kuzingatia program hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button