WAZEE ,machifu na viongozi wa dini mkoani Shinyanga wameunga mkono maridhiano ya mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DP World kutoka Dubai.
Tamko hilo limetolewa Juni 16, 2023 na Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa shinyanga, Charles Njange wakati akisoma tamko la pamoja baina ya viongozi wa dini, wazee na machifu kuhusu kuunga mkono juhudi za serikali katika uwekezaji wa bandari.
“Tunaunga na kuridhia juu ya serikali ya mama samia ya kukuza uchumi na tuko tayari kuwa mabalozi kwa kuelimisha wananchi katika maeneo yetu kwa kuondoa hofu ya upotiloshwaji unaofanywa na baadhi wa watu.
“amesema Kidola.
Viongozi wa dini, wazee na machifu wametoa tamko hilo baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa shinyanga na taarifa maaalum ya uwekazaji wa bandari iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme.
Mndeme aliwasilisha taarifa maalumu ya kuongeza uelewa kuhusu nia na mafanikio tarajiwa ya uwekezaji juu ya ukweli kuhusu maamzui ya serikali dhidi ya upotoshaji unafanywa na watu kwa chuki na kuchoganisha serikali na wananchi.
Mndeme alisema baadhi ya mafanikio ni pamoja na mizigo kushushwa kwa muda mfupi,ajira kuongezeka,mapato kuongezeka,miradi ya mkakati kujengwa na bandari kufikia hadhi ya kimataifa ya vipimo vya utoaji huduma kwa masaa 24.
“Rais samia hawezi kuuza nchi toka imesisiwa na Hayati Mwalimu nyerere na karume,hataweza kutenda jambo hili kwani ana nia njema ya maendeleo kwa watanzania”alisema Mndeme.
” Mkoa wa shinyanga ni mdau mkubwa uwekezaji wa bandari kwa kuunganisha nchi za sudani,congo na Ruanda kwa mizigo ya bandari kupita hapa na tumepanga kuanzisha Samia Economic zone kwa ajili ya kituo maalum cha usafirishaji wa bidhaa kwenda nchi za jirani na hii itachochea ukuaji wa uchumi alisema Mndeme.
,Francian Bahame na Wilson Mashishanga kutoka baraza la wazee wilayani kishapu walishauri serikali kuendelea na utendaji kazi bila kuhofia maneno ya upotoshaji.