‘Wazee wasilipe nauli kwenye pantoni’

BARAZA la Ushauri la Wazee, Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni, Dare s Salaam linapendekeza kuondolewa kwa nauli ya kivuko kwa wazee wote, lakini pia serikali ichukue hatua kali za kisheria kwa watu wanaokiuka na kuwafanyia wazee ukatili.

Limesema ukatili huo ni pamoja na kuwatelekeza, kuwabaka kuwanyang’anya mali zao haswa wanapostaafu, kuwabaka na baadhi yao kuwafanya kitega uchumi kwa kuwatuma kufanya shughuli za ombaomba.

Hayo yamesemwa na Katibu Baraza la Wazee, Wilaya ya Kigamboni, Veronica Nyande katika maadhimisho ya siku ya wazee katika wilaya hiyo na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya, Halima Bulembo.

Advertisement

Akisoma risala ya wazee mbele ya Mkuu wa Wilaya, Nyande amesema pia wazee wanaiomba serikali kuongeza bajeti ya bima ya afya kwa kuwa inayotumika ya CHF, haikidhi kwani wanaweza kukosa baadhi ya huduma ikiwemo dawa na kuomba kutoa fedha za kujikimu kwa wazee, ili kupunguza makali ya maisha.

Kwa upande wake Bulembo amesema lengo la maadhimisho ya wazee ni kuwakutanisha, kutambuana na kujadili changamoto na mafanikio kwa kundi hilo.

Amesema kwa kuadhimisha siku hiyo wazee wameweza kufanyiwa uchunguzi wa afya bure, kupata huduma za lishe na pi ahuduma za kisheria.

“Serikali inatambua uwepo wa wazee ndio maana kuna mabraza ya kata katika ngazi mbalimbali hivyo haina budi kuyatumia kutoa michango na kero zinazowakabili,” amesema Bulembo.

Kuhusu malalamiko na maombi yaliyotolewa na wazee ameahidi kuyachukua na kuyafanyia kazi na kwa suala la tozo ya kivuko kuondolewa alimuagiza Katibu Tawala wa Wilaya kufuatilia.

Kwa upande wake Agnes kisala kutoka shirika la HDT, akizungumza , kwa niaba ya Mkurugenzi , shirika limekuwa likiwaunganisha wazee katika nyanja mbalimbali ilikujua hali zao, kero na namna ya kupata ufumbuzi.

5 comments

Comments are closed.