Wazindua droo ya nne ya ‘Upige Mwingi Afcon’

KAMPUNI ya mtandao wa Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Tecno imezindua droo ya nne ya ‘Upige Mpaka Afcon’ inayotoa fursa kwa jamii kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo tiketi za kwenda kushuhudia fainali za Afcon nchini Ivory coast.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwenye droo ya kusaka washindi wa kampeni hiyo leo, Meneja Mahusiano wa Airtel Jennifer Mbuya alisema kampeni hiyo iliyoanza Januari imeshawanufaisha zaidi ya Watanzania 20 na kwamba itafanyika kwa siku 90.

Alisema mpaka sasa wametoa zawadi mbalimbali kama Smart TV, simu za Tecno Spark 20 na kuna zawadi za pikipiki, jokofu, muda wa maongezi na safari ya kuelekea kwenye fainali za Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Advertisement

“Zawadi zote hizi Watanzania wanaweza kunuifaika kwa kununua muda wa maongezi, kujiunga na vifurushi mbalimbali na kutumia huduma za Airtel,”alisema.

Alisema wiki hii watatangazwa washindi watakaoenda Ivory Coast kushuhudia fainali za Afrika. Kwasasa imefikia hatua ya nusu fainali ambapo timu nne zinatarajiwa kucheza leo kuisaka fainali ambazo ni Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini na Ivory Coast.

Mbuya alisema kupitia kampeni hiyo wanatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya watanzania 90 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Aliwataja baadhi ya walioshinda zawadi za simu za Tecno Spark 20 kuwa ni Yusuf Maneno wa Kigoma (Kasulu), Lameck Jonas Dodoma, Emmanuel Magwina wa Singida (Manyoni). Wengine kutoka Dar es Salaam ni Ally Zungo, Sofia Mnyuwaki, Maisa Omar na Edwin Kimaro.

Meneja Masoko wa Tecno Salma Shafii, alisema ushirikiano wao na Airtel umelenga kuchangia maendeleo katika jamii ya Kitanzania.

” Kila Tecno Spark 20 inapouzwa, tunachangia ustawi na makuzi ya watoto wa Kitanzania, kukuza kupenda michezo na mazoezi ya viungo.”