Waziri aeleza faida malipo kwa mtandao

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Saada Mkuya Salum amesema kuzinduliwa kwa mfumo wa kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa Airpay Tanzania utaisaidia noti ya Tanzania kuwa katika mzunguko kwa muda mrefu.

Aliyasema hayo jana wakati akimwakilisha Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika uzinduzi wa mfumo wa kampuni hiyo, Airpay Tanzania uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Mtandao wa Idara ya Ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) uliofanyika mjini Unguja.

Alisema mfumo wa Airpay utasaidia kupunguza matumizi ya fedha taslimu sokoni, badala yake kutumia mtandao ambapo utasaidia kuiwezesha fedha kutochakaa wala serikali kupata hasara ya kuzalisha fedha mpya kila mara.

Aidha, alisema mfumo huo utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kutumia mfumo wa kidijiti wa kufanya malipo pamoja na kuongeza usalama wa fedha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga amesema kuwa mfumo wa malipo uliozinduliwa utachangia ukuaji wa uchumi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Kampuni ya Airpay, Kunal Jhunjhunwala alisema: “Lengo letu tunataka kumfikia mtu wa kawaida na kwa jinsi Zanzibar inavyoendelea tumeona ni mahali sahihi kuja kuwekeza, tunataka kutoa huduma bora katika nchi zaidi ya 12.”

 

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button